r

ASANTE KWA KUNIAMINI

Jumatatu, 5 Oktoba 2015

HIZI NDIZO SIFA ZA KIONGOZI BORA NA HAWA WANAZO KWA MAENDELEO YA IRINGA NA TANZANIA.

Mbunge wa vitimaalumu Mkoa wa Iringa Rose Tweve akiwa na Mgombea Ubunge Jimbo la Mafinga Bw Cosato Chumi wa pili kulia.
Awaze mafanikio makubwa
Kiongozi bora lazima awe na maono ya juu ya kuhakikisha kuwa nchi yake, kampuni yake sekta yake inapata mafanikio makubwa, hii ndiyo itakuwa dira ya kazi yake itakayompa muongozo wa kusimamia wafanyakazi na watendaji wote walio chini yake kufikia kiwango cha mafanikio anachokiwaza. Kiongozi asiyekuwa na mawazo ya juu ya kuendelea kutoka mahali alipo hafai.

Awe na nia
Haitoshi kwa kiongozi kuwa na mawazo chanya peke yake bila kuwa na nia ya kuyatimiza. Hivyo, kiongozi atafaa kuchaguliwa kuwa kiongozi endapo tu atakuwa na uwezo wa kuratibu vema na kutekeleza alichowaza. Ajue njia anayopita, awatangulie anaowaongoza kwa vitendo. 

Ajitambue mwenyewe
Lazima kiongozi ajitambue mwenyewe ni mtu wa namna gani, ajue uwezo wake na upungufu wake na awe tayari kujiongezea maarifa kila siku, ili aweze kukabili changamoto na mabadiliko ya ulimwengu. Asome, afuatilie mambo yanavyokwenda na ajifunze kwa wenzake kuhusu kufanikisha malengo yake.

Asimamie maamuzi
Kuna wakati malengo hukumbana na vikwazo, hivyo ni wajibu wa kiongozi kusimamia maamuzi sahihi na kuwa mtu wa mwisho. Kiongozi mwenye kubadilika badilika kama kinyonga, hafai kwa vile kukosa msimamo kuna maanisha udhaifu wa mipango na kujiamini.

Adhibiti msongo wa mawazo
Tunamtarajia kiongozi mzuri awe ni mtu mwenye kupunguza msongo wa mawazo, ili kuifanya akili yake ifikie maamuzi sahihi, lakini kama atakuwa mwenye kuwaza mengi, atajikuta anachanganyikiwa na kuwa mtu wa jazba katika maamuzi na hivyo kuipotosha jamii.

Akubali kukosolewa
Viongozi wasiokuwa na sifa za uongozi huwa hawakubali kukosolewa, wakidhani kuwa hiyo ndiyo njia ya kuthibitisha msimamo wao na usahihi wao. Kiongozi makini ni yule ambaye atakuwa tayari kukosolewa na kuwapongeza wanaomkosoa kwa kutazama mwenendo wake na usahihi wake. Asiyekubali kukosolewa hafai kuwa kiongozi.

Awe msikilizaji
Kiongozi mzuri ni yule ambaye atakuwa tayari kuwasilikiza watu walio chini yake, apokee maoni yao na ikiwezekana ayafanyie kazi. Lakini pia anatakiwa kuwafahamu kwa undani, ili aweze kuwaongoza vema kufuatana na hali zao. Akiwa na watu walemavu wenye kasoro kadhaa wa kadhaa anatakiwa kuwatambua kabla na baada ya kuwa kiongozi wao. Kuongoza usichokifahamu ni ujinga.

Afuate haki
Kiongozi imara anatakiwa kufuata haki katika kuongoza kwake, asijione mwenye haki zaidi ya wale anaowaongoza katika sheria. Ni muhimu kwake kuwafanya walio chini yake kujiona wako huru katika mawazo na matendo. Kiongozi anayetumia nguvu na ukali kuongoza watu hafai. Hata yule mwenye kujivunia uongozi wake naye hafai.

Awe egemeo la watu
Sifa nyingine ya kiongozi ni kuwa egemeo la watu wake katika shida na raha. Kiongozi mzuri ni yule ambaye atakuwa tayari kusikitika, kuomboleza, kufurahi pamoja na watu wa chini yake bila kujitenga nao. Ajitolee kuwatumikia watu kwa hali na mali na awe tayari kutumika zaidi kwa maslahi ya wengine.

Atie moyo watu
Kiongozi mzuri ni yule ambaye atakuwa na uwezo wa kuwatia moyo walio chini yake ili waweze kuendeleza vipaji vyao. Haipendezi kwa kiongozi kuwavunja moyo watu kwa kauli za kudharau kazi na jitihada zao walizojaribu kufanya katika kutekeleza majukumu yao kama wafanyakazi au wananchi.

Afurahie mafanikio
Sifa nyingine muhimu ya kiongozi ni kuwa tayari kufurahia mafanikio aliyopata pamoja na watu wake. Ni wajibu wa kiongozi kutoa tuzo, kuwashukuru wafanyakazi wake na kuwa tayari kuwapa ofa. Hii itasaidia kuwafanya watu waone hawajapoteza nguvu zao katika utendaji wao na kwamba wanakubalika. Si busara wakati mwingine kuwakosoa watu mbele ya hadhara na kueleza kutofurahishwa na kazi zao.

Aungane na wa chini yake
Mtu kuwa kiongozi haimaanishi amekuwa wa tofauti na watu wengine kiasi cha kushindwa kuchangamana nao kama wanavyofanya baadhi ya viongozi. Kiongozi mwema ni yule atakayeungana na watu wake katika maisha ya kawaida. Kuwa kiongozi haimaanishi kwamba watu watakufuata wewe kila siku, wakati mwingine wewe unatakiwa kuwafuata wao na kuwa nyuma yao hata mahali walipokosea au wanapokabiliwa na makosa, watetee na uoneshe kuwajali na kuwapigania, makosa utayahesabu baada ya utetezi wako kukamilika.

Akubali lawama
Kama kiongozi amefanya mambo ambayo jamii haikupendezwa nayo anachotakiwa kufanya ni kukubali kulaumiwa. Ikiwa anaongoza kitego cha umeme kwa mfano na watu hawakupata nishati hiyo kwa wakati hatakiwi kukwepa lawama, vivyo hivyo kwenye wizara na idara au nchi kwa ujumla.

Afahamu kutatua matatizo

Kiongozi mzuri ni yule ambaye atakuwa na uwezo wa kuzuia migogoro na kuitatua kwa haraka. Muongozo mzuri katika eneo hili umesimama katika mawasiliano na watu wa chini, mawasiliano haya ndiyo yatakayomuwezesha kiongozi kujua matatizo waliyonayo wafanyakazi wake au hata jamii anayoiongoza na hivyo kumfanya apate wasaa wa kuyashughulikia mapema.

Ajifunze kwa makosa

Wakati mwingine mawazo na mipango inaweza ikaenda kombo, hivyo ni wajibu wa kiongozi kujifunza kutokana na makosa yake au ya wale anaowaongoza, ili kuepuka kurudia makosa yale yale na kumfanya apoteze sifa za kuwa kiongozi mzuri.
Mwanafalsafa Winston Churchill aliwahi kusema "The price of greatness is responsibility." Thamani ya ukuu ni uwajibikaji.
Awe mwaminifu
Miongoni mwa maeneo magumu kabisa yaliyowashinda na yanayoendelea kuwashinda viongozi wengi ni uaminifu. Kiongozi bora ni yule ambaye yuko tayari kusimamia muongozo wa katiba ya nchi au marufuku alizowekewa katika madaraka yake. Hii inakwenda sambamba na kutowaonea, kuwanyanyasa wa nchini yake kwa kutumia cheo chake. 

Awe mkweli
Viongozi wengi hasa wa kisiasa siku hizi ni waongo hakuna mfano, wamejaa ahadi zisizotekelezeka na hata wanapogundua kuwa hawana uwezo au wamekwama kuzitimiza, hawaoni haja ya kutubu mbele ya wanaowaongoza. Kiongozi makini ni yule atayekuwa tayari kuonesha ubora wa matendo na kauli zake.

Asiwe mwenye majungu

Kuna baadhi ya viongozi kwenye maofisi wanaendekeza sana majungu na pengine kuyapa umuhimu wa hali ya juu. Hii ni sifa mbaya kwa kiongozi yo yote, hivyo anayetumikia ‘umbea’ katika ofisi aliyokabidhiwa kama mkuu anapaswa kuondolewa. Kiongozi makini atatumia uwezo wake kuzuia watu wasimsengenye/wasisengenyane kwa kuwa muwazi na mwenye kufungua milango ya watu kumuona na kumlaumu na kueleza hisia zao.

Awe bora
Kwa kila analofanya kama kiongozi lazima alifanye kwa ubora, asiwe mtu mwenye kulipua kazi na kufanya chini ya kiwango cha uwezo wake. Kila siku katika kazi, maamuzi, usimamizi, utekelezaji lazima atumike zaidi ya uwezo wake.

Jumatatu, 28 Septemba 2015

Jumamosi, 26 Septemba 2015

MBUNGE ROSE TWEVE AWATAKA WANANCHI WAWAPUUZE WAPINZANI

Mbunge wa vitimaalum mkoani Iringa Rose Tweve akisalimiana na wapigakura wa jimbo la Mufindi Kaskazini
MBUNGE wa Viti Maalum wa CCM wa Mkoa wa Iringa Mh.Rose Tweve amewataka wananchi kuwa na masimamo wa kuhakikisha kuwa wanakichagua Chama cha Mapinduzi ambacho kwa muda wote kimekuwa kikiwafanyia shughuli za maendeleo na kuwataka wananchi wasidanganywe na kasi za vyama vya Upinzani kuwa wengi wa wapinzani wanalenga kufifisha maendeleo na siyo kuleta maendeleo ndani ya nchi.
 
Hayo aliyasema kwa nyakati tofauti alipokuwa katika jimbo la Mufindi Kaskazini wakati akiomba kura za kuwachagua Rais Dkt John Magufuli, Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kaskazini, Bw. Mendrad Kigola na madiwani wa CCM kuwa kupitia chama hicho cha CCM ndipo wananchi wanaweza kupata maendeleo ya kweli ambayo wanasitahili kuyapata katika Nyanja zote zikiwemo kilimo, ujasiliamali, huduma za maji, sekta za ulinzi na usalama na kukuza uchumi.
 
Mh.Rosse Tweve alisema kuwa maendeleo ya kweli yanapatikana kupitia serikali ya CCM ambapo alisema kuwa chama hicho tangia Uhuru wa Mwaka 1961 kimekuwa na mtazamo Chanya kwa kuhakikisha kuwa kinawaunganisha wananchi nje na ndani ya Tanzania ambapo alisema kuwa amani, utulivu, mshikamano pamoja na uelewano uliopo ndani ya Tanzania umejengwa na Waasisi wa Taifa letu akiwemo Mwalimu Julius Nyerere.
 
Alisema kuwa wananchi wanatakiwa kuacha kudanganyika na kutangatanga kwa kuhamahama vyama vya siasa na kuwa upinzani wa Tanzania unalenga kuwanufaisha watu wachache ambapo CCM kupitia Ilani yake ya Uchaguzi inalenga kupambana kwa umakini kabisa ambapo alisema kuwa mipango ya kujenga sekondari kila kata, zahanati kila kijiji, kusambaza sekta za maji, kuwawezesha wananchi bila upendeleo kufanya  shughuli za ujasiliamali, kusambaza umeme, utunzani wa mazingira, usalama wa raia na mali zao ambapo aliwataka wananchi kuacha kudanganyika kwa kuhamasishwa kuwa upinzani utaweze kuleta maendeleo kwa kasi na kuwa wananchi wanatakiwa kuwa makini.
 
Alisema kuwa endapo kiongozi wa Urais atakuwa safi, atakuwa mpenda maendeleo, atakuwa siyo fisadi, atakuwa mwadilifu, atakuwa anafanya shughuli za maendeleo kwa wananchi wake na kueleza siasa za kweli kwa wananchi wake CCM ndiyo chama pekee kinachoweza kuleta mafanikio yenye mwelekeo kwa wananchi na kuwataka wananchi wawe na msimamo mmoja wa kuichagua CCM kwa kuwa ndiyo chama pekee ambacho kinaweza kutokana na kuwa na Ilani, sababu, nia na uwezo mkubwa wa kuhakikisha kuwa wanapambana na shughuli za kufanikisha kuleta maendeleo ndani ya nchi ya Tanzania.
 
Aliwataka vijana kuhakikisha kuwa wanafanya kazi na kuachana na tabia za kukaa vijiweni wakitegemea vyama vya upinzani kuwa vitawaletea maendeleo ambapo alisema kuwa maendeleo hayawezei kuletwa bali yanakuja kutokana na watu kufanya kazi kwa kujituma, kufanya kazi kwa bidii, kuwa na malengo ambayo yanalenga kuwatoa hatua moja na kwenda hatua nyingine ambapo alisema kuwa vijana wasiote ndoto za mchana kuwa Ukawa utaleta maendeleo bali maendeleo yanaletwa na mtu kwa kufanya kazi kwa kujituma, kuwa na mikakati, kuwa na mipango na uwezeshaji ambapo alisema kuwa CCM ndiyo chama pekee ambacho kinaweza kuwawezesha wananchi wake na wakafanya shughuli za maendeleo bila usumbufu.
 

Alisema kuwa vijana wanatakiwa wasidanganywe kwa kuuchagua upinzani ambapo alisema kuwa endapo watafanya makosa watajutia maisha yao yote na kuwa vijana wanatakiwa kutambua kuwa kuwa na msimamo, kuwa na mikakati, kuwa na mwlekeo, kuwa na mipango na kuwa na malengo ndiko pekee ambako kunaweza kuwaendeleza wananchi wake kwa kuwaletea maendeleo ya kweli.

Jumatano, 23 Septemba 2015

Jumanne, 22 Septemba 2015

MBUNGE WA VITIMAALUM AWATAKA WANANCHI WA JIMBO LA MAFINGA KUMCHAGUA COSATO CHUMI KWA MAENDELEO.

Mbunge wa vitimaalum Rose Tweve akiwa na Mgombea ubunge Jimbo la Mafinga Mjini(CCM)Bw Cosato Chumi wakiwa na wapiga kura.
Mgombea Ubunge Jimbo la Mafinga Mjini Bw Cosato Chumi akiwa na wapigakura.
Mgombea Ubunge Mafinga Mjini akiwa na viongozi wa Chama cha mapinduzi wilaya

Jumanne, 1 Septemba 2015

WANAWAKE NCHI WAMEASWA KUKIUNGA MKONO CHAMA CHA MAPINDUZI ILI KIWESHE KUSHINDA KATIKA UCHAGUZI MKUU WA OCT 25 MWAKA ILI KIENDELEE KUWAPA MAENDELEO WANANCHI.

Mbunge wa vitimaalum Rose Tweve akisalimiana na diwani wa kata ya makolongoni anayejilikana kwa jina la Tenga wakiwa katika ofisi za kata.
Mbunge wa vitimaalum mkoa wa Iringa Rose Tweve akiagana na wanawake wa kata ya Makolongo manispaa ya Iringa.

Wanawake wameaswa kukipenda chama cha mapinduzi kwakuwa ndicho chama pekee kitakachowaletea maendeleo yanayotakiwa kwakuwa kinajua changamoto zinazo wakabili wananchi katika kipindi hiki.
   Akizungunguza na  wanawake wa wa Kata ya Makolongoni Mbunge wa viti maalum mkoani Iringa Rose Tweve  aliwataka wananchi kutobabaishwa na wapinzani kwani hawana nia njema na watanzania  na kusema kuwa chama hicho kina misingi ya kutetea amani ya Nchi.
   Alisema huu ndiyo wakati wa wanawake kujitokeza kwa wingi kukiunga mkono chama cha mapinduzi kwa kuwapigia kura wagombea wanaotokana na chama hicho kwakuwa kukipa nchi chama cha Upinzani ni kujisaliti wenyewe hiyo aliwaomba wanawake kuhakikisha wanakisaidia chama cha mapinduzi kiweze kushinda.