Mbunge wa vitimaalium mkoani iringa Rose Tweve akiwa katika mkutano wa Mgombea Urais Dk John Pombe Magufuli Iringa mjini. |
Jumatatu, 28 Septemba 2015
MBUNGE ROSE TWEVE ASHIRIKI KIKAMILIFU KATIKA MIKUTANO YA KAMPENI AAHIDI KUYAFIKIA MAKUNDI MBALIMBALI.
Jumapili, 27 Septemba 2015
Jumamosi, 26 Septemba 2015
MBUNGE ROSE TWEVE AWATAKA WANANCHI WAWAPUUZE WAPINZANI
Mbunge wa vitimaalum mkoani Iringa Rose Tweve akisalimiana na wapigakura wa jimbo la Mufindi Kaskazini |
MBUNGE wa Viti Maalum wa CCM wa Mkoa wa Iringa Mh.Rose Tweve amewataka wananchi kuwa na masimamo wa kuhakikisha kuwa wanakichagua Chama cha Mapinduzi ambacho kwa muda wote kimekuwa kikiwafanyia shughuli za maendeleo na kuwataka wananchi wasidanganywe na kasi za vyama vya Upinzani kuwa wengi wa wapinzani wanalenga kufifisha maendeleo na siyo kuleta maendeleo ndani ya nchi.
Hayo aliyasema kwa nyakati tofauti alipokuwa katika jimbo la Mufindi Kaskazini wakati akiomba kura za kuwachagua Rais Dkt John Magufuli, Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kaskazini, Bw. Mendrad Kigola na madiwani wa CCM kuwa kupitia chama hicho cha CCM ndipo wananchi wanaweza kupata maendeleo ya kweli ambayo wanasitahili kuyapata katika Nyanja zote zikiwemo kilimo, ujasiliamali, huduma za maji, sekta za ulinzi na usalama na kukuza uchumi.
Mh.Rosse Tweve alisema kuwa maendeleo ya kweli yanapatikana kupitia serikali ya CCM ambapo alisema kuwa chama hicho tangia Uhuru wa Mwaka 1961 kimekuwa na mtazamo Chanya kwa kuhakikisha kuwa kinawaunganisha wananchi nje na ndani ya Tanzania ambapo alisema kuwa amani, utulivu, mshikamano pamoja na uelewano uliopo ndani ya Tanzania umejengwa na Waasisi wa Taifa letu akiwemo Mwalimu Julius Nyerere.
Alisema kuwa wananchi wanatakiwa kuacha kudanganyika na kutangatanga kwa kuhamahama vyama vya siasa na kuwa upinzani wa Tanzania unalenga kuwanufaisha watu wachache ambapo CCM kupitia Ilani yake ya Uchaguzi inalenga kupambana kwa umakini kabisa ambapo alisema kuwa mipango ya kujenga sekondari kila kata, zahanati kila kijiji, kusambaza sekta za maji, kuwawezesha wananchi bila upendeleo kufanya shughuli za ujasiliamali, kusambaza umeme, utunzani wa mazingira, usalama wa raia na mali zao ambapo aliwataka wananchi kuacha kudanganyika kwa kuhamasishwa kuwa upinzani utaweze kuleta maendeleo kwa kasi na kuwa wananchi wanatakiwa kuwa makini.
Alisema kuwa endapo kiongozi wa Urais atakuwa safi, atakuwa mpenda maendeleo, atakuwa siyo fisadi, atakuwa mwadilifu, atakuwa anafanya shughuli za maendeleo kwa wananchi wake na kueleza siasa za kweli kwa wananchi wake CCM ndiyo chama pekee kinachoweza kuleta mafanikio yenye mwelekeo kwa wananchi na kuwataka wananchi wawe na msimamo mmoja wa kuichagua CCM kwa kuwa ndiyo chama pekee ambacho kinaweza kutokana na kuwa na Ilani, sababu, nia na uwezo mkubwa wa kuhakikisha kuwa wanapambana na shughuli za kufanikisha kuleta maendeleo ndani ya nchi ya Tanzania.
Aliwataka vijana kuhakikisha kuwa wanafanya kazi na kuachana na tabia za kukaa vijiweni wakitegemea vyama vya upinzani kuwa vitawaletea maendeleo ambapo alisema kuwa maendeleo hayawezei kuletwa bali yanakuja kutokana na watu kufanya kazi kwa kujituma, kufanya kazi kwa bidii, kuwa na malengo ambayo yanalenga kuwatoa hatua moja na kwenda hatua nyingine ambapo alisema kuwa vijana wasiote ndoto za mchana kuwa Ukawa utaleta maendeleo bali maendeleo yanaletwa na mtu kwa kufanya kazi kwa kujituma, kuwa na mikakati, kuwa na mipango na uwezeshaji ambapo alisema kuwa CCM ndiyo chama pekee ambacho kinaweza kuwawezesha wananchi wake na wakafanya shughuli za maendeleo bila usumbufu.
Alisema kuwa vijana wanatakiwa wasidanganywe kwa kuuchagua upinzani ambapo alisema kuwa endapo watafanya makosa watajutia maisha yao yote na kuwa vijana wanatakiwa kutambua kuwa kuwa na msimamo, kuwa na mikakati, kuwa na mwlekeo, kuwa na mipango na kuwa na malengo ndiko pekee ambako kunaweza kuwaendeleza wananchi wake kwa kuwaletea maendeleo ya kweli.
Jumatano, 23 Septemba 2015
MKOA WA IRINGA WAPATA JEMBE JINGINE KWAAJILI YA WANAWAKE MBADALA WA LEDIANA MNG'ONG'O AMBAYE NI ROSE TWEVE.
Jumanne, 22 Septemba 2015
MBUNGE WA VITIMAALUM AWATAKA WANANCHI WA JIMBO LA MAFINGA KUMCHAGUA COSATO CHUMI KWA MAENDELEO.
Jumanne, 8 Septemba 2015
Jumanne, 1 Septemba 2015
WANAWAKE NCHI WAMEASWA KUKIUNGA MKONO CHAMA CHA MAPINDUZI ILI KIWESHE KUSHINDA KATIKA UCHAGUZI MKUU WA OCT 25 MWAKA ILI KIENDELEE KUWAPA MAENDELEO WANANCHI.
Mbunge wa vitimaalum Rose Tweve akisalimiana na diwani wa kata ya makolongoni anayejilikana kwa jina la Tenga wakiwa katika ofisi za kata. |
Mbunge wa vitimaalum mkoa wa Iringa Rose Tweve akiagana na wanawake wa kata ya Makolongo manispaa ya Iringa. |
Wanawake wameaswa kukipenda chama cha mapinduzi kwakuwa ndicho chama pekee kitakachowaletea maendeleo yanayotakiwa kwakuwa kinajua changamoto zinazo wakabili wananchi katika kipindi hiki.
Akizungunguza na
wanawake wa wa Kata ya Makolongoni Mbunge wa viti maalum mkoani Iringa
Rose Tweve aliwataka wananchi
kutobabaishwa na wapinzani kwani hawana nia njema na watanzania na kusema kuwa chama hicho kina misingi ya
kutetea amani ya Nchi.
Alisema huu ndiyo wakati wa wanawake kujitokeza kwa wingi
kukiunga mkono chama cha mapinduzi kwa kuwapigia kura wagombea wanaotokana na
chama hicho kwakuwa kukipa nchi chama cha Upinzani ni kujisaliti wenyewe hiyo
aliwaomba wanawake kuhakikisha wanakisaidia chama cha mapinduzi kiweze
kushinda.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)