r

ASANTE KWA KUNIAMINI

Jumatatu, 4 Aprili 2016

NASHIRIKI KIKAMILIFU KATIKA KAMATI ZETU


picha ya pamoja na wanakamati wenzangu



Kiongozi bora lazima awe na maono ya juu ya kuhakikisha kuwa nchi yake, kampuni yake sekta yake inapata mafanikio makubwa, hii ndiyo itakuwa dira ya kazi yake itakayompa muongozo wa kusimamia wafanyakazi na watendaji wote walio chini yake kufikia kiwango cha mafanikio anachokiwaza. Kiongozi asiyekuwa na mawazo ya juu ya kuendelea kutoka mahali alipo hafai.
Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Iringa (ccm) Mh Rose Tweve ameendelea na majukumu yake ya kibunge jijini Dar es salaam, ambako kunaendelea vikao vya kamati mbalimbali na yeye akiwa miongoni mwa wanakamati za bunge 

Jumapili, 3 Aprili 2016

NILIJUMUIKA NA WANAWAKE WENZANGU SIKU YA WANAWAKE DUNIANI



 

RISARA YA MGENI RASMI MBUNGE WA VITIMAALUMU ROSE TWEVE SIKU YA WANAWAKE 08/03/2015 KIJIJI CHA IGOWOLE WILAYA YA MUFINDI
          Ndugu Viongozi mbalimbali wa Vyama vya Siasa,                                   Watendaji wa Serikali na Asasi za Kiraia,                                                     Viongozi wa Jumuiya za Dini,                                                                              Waandishi wa Habari,                                                                      Wakina Mama wote,                                                                         Wageni waalikwa,                                                                                      Mabibi na Mabwana.
Ndugu viongozi na wananchi wote mliohudhuria.Napenda kuchukua fursa hii kuushukuru uongozi wa Wilaya ya Mufindi  pamoja na Viongozi wote wa Serikali kwa ujumla kwa maandalizi mazuri kufanikisha shughuli hii ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani mwaka huu 2016 inayofanyika kiwilaya  hapa Igowole.
Niwashukuru kwa dhati wananchi wote wa wilaya hii, kwa namna mlivyojipanga kwa kushirikisha akina mama, vikundi mbalimbali vya sanaa na burudani kufanikisha Maadhimisho haya.

NIMEWAWEZESHA AKINA MAMA WAJASILIAMALI.



Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Iringa (ccm) Rose Tweve ameendelea kukutana na makundi mbalimbali katika mkoa huo, mwishoni mwa wiki hili amekutana na wajasiliamali wanawake katika makundi mawili tofauti. Kundi la kwanza alilokutana nalo ni lile la umoja wa wanawake wa ccm Iringa mjini, waliounda vicoba kwa ajili ya kukopeshana na kuendeleza miradi kadhaa ya kijasiliamali.
Aidha wanawake hao wakati wakisoma risala kwa mbunge huyo wamesema kuwa wanakabiliana na changamoto kadhaa hasa ukosefu wa mtaji utakao wafanya waendeleze vicoba hivyo ambavyo imekuwa kimbilio la makundi mbalimbali mijini na vijijini.



Pia wanawake wao wamemwomba mbunge huyo kuhakikisha kuwa wanawake wa mkoa wa Iringa wanakuwa mfano wa kuigwa katika kuanzisha, kukilinda na kukitetea chama chao hicho cha vicoba kwa kuwa vinaonesha nia ya kuwasaidia kujikimu kimaisha, mpaka sasa wameanza kutafuta wataalamu wa kufundisha namna ya kufuga kuku ili wapate elimu sahihi na kasha kuanza kutekeleza mladi huo.
Kwa upande wake mbunge huyo kijana ametoa milioni moja taslimu kama mkopo usiokuwa na riba ili uweze kuwasaidia kuendeleza mtaji wao pia akatumia fursa hiyo kuwaomba mkopo huo wauzungushe katika miradi mbalimbali kama ya ufugaji kuku n.k. pia ameonesha nia ya kuwasaidia wanawake hao na kuwaahidi kuwa wakiwa na uaminifu wa kulinda mtaji wao hata kama ni mdogo atahakikisha kuwa vicoba hiyo inakuwa ya mfano wa kuigwa mkoani Iringa.