r

ASANTE KWA KUNIAMINI

Jumapili, 12 Machi 2017

Matukio katika picha ziara ya wilaya ya Kilolo mkoa wa Iringa

wiki lililo pita nilifanya ziara ya kuwatembelea wanawake wa wilaya ya kilolo, Mkoani Iringa. nilipata fursa ya kutembelea kata nne ambapo nilikutana na akina mama wenzangu na kuzungumza masuala mbalimbali yanayo husu kujikwamua kiuchumi. Miongoni kata hizo ni pamoja na KISINGA,  IHIMBO, NG`ULUWE na MLAFU.
  Taarifa rasmi za kile ambacho nimekifanya nitawaletea mwishoni mwa mwezi huu.


 Baada ya ibada kata ya ihimbo nilifanikiwa kuongea na wananchi wa kaya hiyo


 nikimsikiliza Katibu wangu Neema Nyasi diwani wa viti maalumu wilaya ya kilolo, wakati wa Ibada katika kanisa la KKKT kata ya Ihimbo


Jumatatu, 30 Januari 2017

MBUNGE VITI MAALUM IRINGA ROSE TWEVE AFANYA ZIARA KATIKA KATA MBILI ZA MKOA HUO




Na sebastian emmanuel, iringa
Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Iringa Rose Tweve ameanza rasmi kutimiza ahadi zake za kusikiliza kero za wananchi pamoja na kuangalia namna ya kuwasaidia wakina mama wa mkoa huo kujiinua kiuchumi.

Katika ziara hiyo mbunge huyo wa viti maalum mkoa wa Iringa kupitia Chama cha mapinduzi (CCM) Rose ameanza kutimiza ahadi zake alizowaahidi wananchi wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka 2015 ndani ya jumuiya ya UWT mkoa wa Iringa.

Ziara yake ya kwanza imeanza Januari 28 2017 katika wilaya ya Kilolo mkoani Iringa na kutembelea kata za Mtitu na Ukumbi na aliweza kuongozana na mbunge viti maalumu kutoka mkoa wa Songwe Juliana Shonzana pamoja na viongozi wa UWT wilaya ya Kilolo.

Pamoja na mambo mengine Rose ametoa jumla ya shilingi za kitanzania milioni moja na laki tisa ( 1,900,000) kwa jumuiya ya akina mama (UWT) wilaya ya Kilolo kwa ajili ya kujiimarisha na kuinua vikundi vya vya akina mama wa jumuiya hiyo. 

Rose anaamini kuwa UWT ni kiungo kikubwa na muhimu ndani ya Chama cha Mapinduzi hivyo kama jumuiya ikiwa imara kwa kupitia miradi mbali mbali basi italeta hamasa ndani ya chama na ameahidi kuwa ziara hii ni endelevu na itakuwa ya mkoa mzima.


                  tukifurahia jambo

  Mbunge viti maalumu mkoa wa Songwe Juliana Shonzana akipokea zawadi kutoka kwa akinamama wa UWT kata ya Ukumbi katika ziara iliyofanywa na Mbunge wa Viti maalumu mkoa wa Iringa Rose Tweve mwishoni mwa wiki hii.

Jumamosi, 21 Januari 2017

ziarani Mbeya na mpakani mwa Nchi ya malawi


Hivi karibuni tulitembelea mkoa wa Mbeya katika ziara ya kamati ya Bunge ya mambo ya nje, ulinzi na usalama na waziri wa ulinzi Hussein Mwinyi. pia tulitembelea gereza la songwe pamoja na kuangalia mpaka kati ya Malawi na Tanzania.

mbunge wa viti maalumu mkoa wa Songwe (ccm) Juliana Shoza,  akisalianma na moja ya viongozi wa jeshi la magereza la mbeya (Luanda)


Jumanne, 29 Novemba 2016

NILIFANYA ZIARA KWA AKINA MAMA WAJASILIA MALI WA MADUMA

nikipokea zawadi ya kikapu kutoka kwa akina mama hao wa Maduma nilipokwenda kuwatembelea na kuangalia namna wanavyojishughulisha katika biashara zao za ujasiriamali. .

 kama mbunge  wa viti maalum CCM  mkoa wa Iringa, nilipata fursa ya kutembelea kikundi cha akina mama wa kata ya Maduma Wilaya ya Mufindi na kuwapongeza kwa juhudi zao wanazozifanya katika shughuli za ujasiriamali.

Jumatano, 23 Novemba 2016

MWANANCHI, MWANAMKE, WATU WANGU.


 NIKIONGOZANA NA MH. JULIANA SHONZA (MB) WA VITI MAALUMU WA MKOA WA SONGWE WAKATI WA KUHUDHURIA VIKAO VYA MBUNGE MJINI DODOMA.