nikipokea zawadi ya kikapu kutoka kwa akina mama hao wa Maduma nilipokwenda kuwatembelea na kuangalia namna wanavyojishughulisha katika biashara zao za ujasiriamali. .
kama mbunge wa viti maalum CCM mkoa wa Iringa, nilipata fursa ya kutembelea kikundi cha akina mama wa kata ya Maduma Wilaya ya Mufindi na kuwapongeza kwa juhudi zao wanazozifanya katika shughuli za ujasiriamali.
nikikamkabidhi moja ya akina mama wa Maduma fedha taslimu kiasi cha milioni moja kwa ajili ya kuendeleza mitaji yao ya biashara.Katika ziara hiyo, niliongozana na baadhi ya viongozi wa wilaya ya Mufindi na wao waliweza kuchangia Laki tano kwa wakina mama hao. wakati wa kampeni za mwaka jana pamoja na ilani ya chama cha Mapinduzi niliwaahidi wakina mama wa Iringa kuwa ataungana nao katika kuwasaidia kujiinua kiuchumi na kupambana na umaskini kwa Kuanzisha mfuko wa wanawake ambao umeshaanza kufanya kazi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni