Zikiwa
zimebaki siku chache Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kuanza tayari
baadhi ya wabunge wameanza kuingia mkoani humo kwaajili ya maandalizi na
kukutana na wananchi wao na kupokea kero na mambo yanayotakiwa kupelekwa
Bungeni.
Wananchi wanayoshauku kubwa kutaka kuona mwenendo wa Bunge
hili la 11 chini ya usimamizi wa Spika wa Bunge Ndg.Job Ndugai na Naibu Wake Dr
Tulia Akson ambapo wanaamini litajaa hekima na Busara katika kujadili maswala
ya maendeleo ya wananchi bila kubagua aina ya mtu kutokana na aina ya kiongozi
wa nchi yaani Rais Magufuli kuonesha kuwa hana upendeleo na yupo kwaajili ya
kuwatumikia watanzania wote.
Hali hiyo inamfanya mbunge wa vitimaalumu mkoani Iringa
kuona umuhimu wa kuzungumzia suala la nini kitakachofanyika katika kipindi
chake cha miaka mitano ya awali ikiwa anatambua kuwa uongozi ni dhamana
aliyopewa kwaajili ya wengi,"ninaondoka Iringa kwenda dodoma nikiwa najua
changamoto na shida walizonazo wananchi wangu wa Iringa hususani wanawake
katika sekta mbalimbali Afya,Elimu,Maji,Miundombinu na huduma nyinginezo ambazo
kwahakika zinaumiza na kwa kutambua hilo nitafanya kazi kwaajili ya wananchi
jukumu langu kubwa nikuhakikisha nazifikisha changamoto zao mahali panapo
stahili na kuhakikisha zinatatuliwa"alisema rose
Aliiendelea kusema,"kwa muda mrefu sasa wananchi ambao
wametupa dhamana hii ya kuwaongoza wamekuwa wakiishi katika maisha duni ni kama
hawana viongozi inasikitisha pia kuona mkoa wa Iringa uliojaa raslimali nyingi
za misitu na mbuga za wanyama tukaendelea kuishi maisha yaleyele tuliyoishi
enzi hizo ni lazima tuhoji na wananchi wanufaike na mali zao haiwezekani mali
walizoshiriki kuzitafuta,kuzilinda mpaka zilipofikia halafu wakafaidi watu
wageni sasa ni mwenyeji kwanza mgeni baadae hilo ndilo jukumu langu kama
mbunge"alisema
Anasema kumekuwa na tatizo la wanawake wajawazito kukosa
huduma za kujifungua katika hospitali mbalimbali na vituo vya afya jambo ambalo
linatakiwa litafutiwe ufumbuzi huku akisema jukumu la wabunge ni kuihamnasisha
serikali kutenga bajeti itakayotatua baadhi ya kero hususani hiyo ya kuboresha
huduma za afya.
"pamoja na kutambua hali hiyo inayo wakabili wanawake
lipo pia tatizo la huduma hiyohiyo ya afya kwa wazee ambapo serikali ilitangaza
kuwa wezee watatibiwa bure lakini bado ipo changamoto kwa baadhi ya hospitali
na zahanati bado zinaendelea kuwatoza fedha wazee kazi yangu ni kwenda
kufuatilia sheria zinasemaje juu ya jambo hili" alisema rose
Endelea kufuatilia ujue mambo yatakayotekelezwa na Mh Rose
katika kipindi cha miaka mitano ya mwanzo...............asanteni.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni