r

ASANTE KWA KUNIAMINI

Jumatatu, 8 Februari 2016

SHUGHULI MBALIMBALI ZILIZOFANYIKA NA JUMUIYA ZA NDANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI KATIKA KUADHIMISHA MIAAKA 39 YA CCM

Jumuiya ya Wanawake UWT wilaya ya Iringa wakiwa katika kituo cha kulelea wazee kilichopo eneo la Kitanzini manispaa ya Iringa.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi wilaya ya Iringa Ndg.Yahaya Msigwa akiwa na wanajumuiya katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Kiislamu kilichopo Ilala manispaa ya Iringa.
Viongozi wa Chama wilaya ya Mufindi wakiwa kijiji cha Sadani kwaajili ya mkutano wa Hadhara.
Jamii mkoani Iringa imetakiwa kuunga mkono jitihada za serikali na wadau mbalimbali katika katika kwasaidia watu wa makundi maalumu hususani wezee na walemavu waliopo katika maeneo yao.

Imeelezwa kuwa kuwasaidia watu wa makundi hayo ni jukumu la kila mwanchi kutokana na hali zao na mahitaji waliyonayo ambapo itawasaidi kuwajengea matumaini mapya katika maisha yao kama wananvyo eleza Ashura Jongo kaimu mwenyekiti UWT mkoa wa Iringa na Cesilia Ismail katibu UWT wilaya ya Iringa walipotembelea kituo cha kulelea wazee cha MAKHAZINI kilichopo kitanzini Manispaa ya Iringa na kutoa msaada wa vyakula mbalimbali kituoni hapo.

Nao baadhi ya wanajumuiya hiyo ya wanawake wa CCM waliohudhulia katika ziara hiyo wamesema wataendelea kujitolea katika kuwasaidia wazee na wasiojiweza pamoja na kuendelea kwahamasisha wananchi kuunga mkono jitihada zinazofanywa na wanawake wa chama cha mapinduzi hasa katika kipindi hiki cha maadhimisho ya miaka 39 ya CCM.

Bi Hadija Tagalile ni mlezi wa wazee hao amesema wanawake waliopo kituoni hapo ni wale waliokosa msaada kutoka kwa ndugu zao japo katika kituo hicho wakiendelea kupata huduma huku baadhi ya wazee waliopokea msaada huo wakiendelea kuhamasisha jamii kuwatembelea katika kituo hicho.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni