r

ASANTE KWA KUNIAMINI

Jumatatu, 2 Mei 2016

NIMETEKELEZA AHADI,



Ni kwa kikundi cha vikoba cha wanawake uwt iringa mjini, pamoja na kile cha wanawake wanaoishi na ulemavu
Anaandika Sebastian Emmanuel Jr, Mafinga 
Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Iringa (ccm) Mh. Rose Tweve, ametekelza ahadi yake aliyoiahidi mwezi mmoja ulipita kwa wanawake wa kikundi cha wajasilia mali wanaounda kikundi cha (UWT  vikoba na kile cha wanawake wanaoishi na ulemavu Iringa mjini.
 Mbunge huyo kijana wakati alipokwenda kuwatembelea mwezi mmoja uliopita,  aliwaomba watengeneze mchanganuo wa shughuli za kufanya ili aone namna ya kuwasaidia, pamoja na hayo aliwaahidi pesa za kitanzania shilingi milioni mbili kwa vikundi vyote viwili, ili ziweze kuwasaidia katika shughuli zao za kijasiliamali.
Pamoja na mambo mengine mbunge huyo amewakabidhi pesa zote alizo ahidi na kuwaomba waendelee kukopeshana kwa faida ili vikundi vyao visife kama baadhi ya vikundi vingine. Wanawake hao wamemweleza mbunge huyo kuwa watahakikisha kuwa wanatunza mtaji huo ili uwape faida kubwa baadaye, pia walimemweleza mbunge kuwa wameandaa mradi wa kutotoresha vifaranga vya kuku ili waweze kuviuza na mbunge amewaahidi kuwatafutia soko la uhakika.





Hakuna maoni:

Chapisha Maoni