-Ni juu ya mkataba tata wa kampuni ya Rai group inayomiliki kiwanda hicho cha Mufindi Paper Mill's.
-Wadau wilaya ya Mufindi waungana kuibana serikali na kiwanda hicho,
wenyewe wanasema hiyo itakuwa ni agenda ya kudumu mpaka serikali itakapo
amua kulivalia njuga
Anaandika Sebastian Emmanuel jr, Dar es salaam.
Mbunge wa miti maalum mkoa wa Iringa, mh Rose Tweve, wiki hili bungeni
Dodoma aliiuliza serikali swali kupitia wizara ya mali asili na utalii,
inayoongozwa na Mh. Jumanne magembe, kuwa kwanini kampuni ya Rai Group
inayo miliki kiwanda cha karatasi mgololo mpm inatozwa nusu ya bei ya
vibali vya ununuzi wa magogo katika shamba la msitu wa Taifa wa saohill
lililopo wilayani Mufindi, huku wavunaji wa kawaida wanatozwa Bei kubwa
kwa vipimo vile vile, ameomba ufafanuzi wa lini serikali itapitia upya
mkataba wa kampuni hiyo wa uvunaji magogo kwa upendeleo huku ikiwaacha
wananchi na wafanya biashara wengine kuendelea kuuziwa kwa bei kubwa, na
kutozwa bei kubwa amekwenda mbali zaidi kwa kusema kuwa serikali
inakosa mapato makubwa kupitia vibali hivyo kitu ambacho
kinaonekana/kinatafsiliwa kuna jambo nyuma nyuma ya pazia. Amesema kama
ikiwa wananchi watashirikishwa katika kupewa vibali hivyo bila upendeleo
wowote ni hakika uchumi wa wanamufindi na Taifa kwa ujumla utakuwa kwa
Kiwango kikubwa hususani kwa vikundi vya kijasilia mali, vijana, akina
mama na wazee.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni