Jumanne, 29 Novemba 2016
Jumatano, 23 Novemba 2016
MWANANCHI, MWANAMKE, WATU WANGU.
NIKIONGOZANA NA MH. JULIANA SHONZA (MB) WA VITI MAALUMU WA MKOA WA SONGWE WAKATI WA KUHUDHURIA VIKAO VYA MBUNGE MJINI DODOMA.
Ijumaa, 8 Julai 2016
Alhamisi, 2 Juni 2016
KIWANDA CHA KARATASI MGOLOLO MPM CHAZIDI KUANDAMWA.
-Ni juu ya mkataba tata wa kampuni ya Rai group inayomiliki kiwanda hicho cha Mufindi Paper Mill's.
-Wadau wilaya ya Mufindi waungana kuibana serikali na kiwanda hicho,
wenyewe wanasema hiyo itakuwa ni agenda ya kudumu mpaka serikali itakapo
amua kulivalia njuga
Anaandika Sebastian Emmanuel jr, Dar es salaam.
endelea.......
MBUNGE ROSE TWEVE AIKOMALIA SERIKALI MIFUKO YA KUSAIDIA MAENDELEO YA VIJANA,WANAWAKE IRINGA
Mbunge wa Viti Maalum, Rose Tweve (CCM) akiuliza swali kwa Waziri wa Nnchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), bungeni Dodoma , kwamba ni fedha kiasi gani kimetengwa kwa ajili ya maendeleo ya vijana na wanawake mkoani Iringa. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Jumatatu, 2 Mei 2016
NIMETEKELEZA AHADI,
Ni
kwa kikundi cha vikoba cha wanawake uwt iringa mjini, pamoja na kile cha
wanawake wanaoishi na ulemavu
Anaandika
Sebastian Emmanuel Jr, Mafinga
Mbunge
wa viti maalumu mkoa wa Iringa (ccm) Mh. Rose Tweve, ametekelza ahadi yake
aliyoiahidi mwezi mmoja ulipita kwa wanawake wa kikundi cha wajasilia mali
wanaounda kikundi cha (UWT vikoba na
kile cha wanawake wanaoishi na ulemavu Iringa mjini.
Jumatatu, 4 Aprili 2016
NASHIRIKI KIKAMILIFU KATIKA KAMATI ZETU
picha ya pamoja na wanakamati wenzangu
Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Iringa (ccm) Mh Rose Tweve ameendelea na majukumu yake ya kibunge jijini Dar es salaam, ambako kunaendelea vikao vya kamati mbalimbali na yeye akiwa miongoni mwa wanakamati za bunge
Jumapili, 3 Aprili 2016
NILIJUMUIKA NA WANAWAKE WENZANGU SIKU YA WANAWAKE DUNIANI
RISARA
YA MGENI RASMI MBUNGE WA VITIMAALUMU ROSE TWEVE SIKU YA WANAWAKE 08/03/2015
KIJIJI CHA IGOWOLE WILAYA YA MUFINDI
Ndugu
Viongozi mbalimbali wa Vyama vya Siasa, Watendaji
wa Serikali na Asasi za Kiraia, Viongozi
wa Jumuiya za Dini, Waandishi
wa Habari, Wakina
Mama wote, Wageni waalikwa, Mabibi
na Mabwana.
Ndugu viongozi na wananchi wote mliohudhuria.Napenda
kuchukua fursa hii kuushukuru uongozi wa Wilaya ya Mufindi pamoja na Viongozi wote wa Serikali kwa ujumla
kwa maandalizi mazuri kufanikisha shughuli hii ya Maadhimisho ya Siku ya
Wanawake Duniani mwaka huu 2016 inayofanyika kiwilaya hapa Igowole.
Niwashukuru kwa dhati wananchi wote wa wilaya
hii, kwa namna mlivyojipanga kwa kushirikisha akina mama, vikundi mbalimbali
vya sanaa na burudani kufanikisha Maadhimisho haya.
NIMEWAWEZESHA AKINA MAMA WAJASILIAMALI.
Mbunge wa viti maalumu mkoa wa
Iringa (ccm) Rose Tweve ameendelea kukutana na makundi mbalimbali katika mkoa
huo, mwishoni mwa wiki hili amekutana na wajasiliamali wanawake katika makundi
mawili tofauti. Kundi la kwanza alilokutana nalo ni lile la umoja wa wanawake
wa ccm Iringa mjini, waliounda vicoba kwa ajili ya kukopeshana na kuendeleza
miradi kadhaa ya kijasiliamali.
Aidha wanawake hao wakati wakisoma
risala kwa mbunge huyo wamesema kuwa wanakabiliana na changamoto kadhaa hasa
ukosefu wa mtaji utakao wafanya waendeleze vicoba hivyo ambavyo imekuwa
kimbilio la makundi mbalimbali mijini na vijijini.
Pia wanawake wao wamemwomba mbunge
huyo kuhakikisha kuwa wanawake wa mkoa wa Iringa wanakuwa mfano wa kuigwa
katika kuanzisha, kukilinda na kukitetea chama chao hicho cha vicoba kwa kuwa
vinaonesha nia ya kuwasaidia kujikimu kimaisha, mpaka sasa wameanza kutafuta
wataalamu wa kufundisha namna ya kufuga kuku ili wapate elimu sahihi na kasha
kuanza kutekeleza mladi huo.
Kwa upande wake mbunge huyo kijana
ametoa milioni moja taslimu kama mkopo usiokuwa na riba ili uweze kuwasaidia
kuendeleza mtaji wao pia akatumia fursa hiyo kuwaomba mkopo huo wauzungushe
katika miradi mbalimbali kama ya ufugaji kuku n.k. pia ameonesha nia ya
kuwasaidia wanawake hao na kuwaahidi kuwa wakiwa na uaminifu wa kulinda mtaji
wao hata kama ni mdogo atahakikisha kuwa vicoba hiyo inakuwa ya mfano wa kuigwa
mkoani Iringa.
Jumamosi, 20 Februari 2016
MBUNGE WA VITI MAALUM MKOANI RINGA ROSE TWEVE AWATAKA WANAWAKE KUSHIRIKIANA NA KUJITUMA ILI KUJILETEA MAENDELEO
Mh.Mbunge wa Vitimaalumu mkoani Iringa(ccm) Rose Tweve akizungumza kwa msisitizo katika baraza la wanawake wilaya ya Iringa. |
Mh.Rose akiwasalimia baadhi ya wajumbe wa UWT Iringa vijijini katika viwanja vya ccm sabasaba Iringa |
Viongozi wa UWT wilaya ya Iringa wakiwa na Mbunge wa vitimaalumu Rose Tweve |
Jumatatu, 8 Februari 2016
SHUGHULI MBALIMBALI ZILIZOFANYIKA NA JUMUIYA ZA NDANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI KATIKA KUADHIMISHA MIAAKA 39 YA CCM
Jumuiya ya Wanawake UWT wilaya ya Iringa wakiwa katika kituo cha kulelea wazee kilichopo eneo la Kitanzini manispaa ya Iringa. |
Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi wilaya ya Iringa Ndg.Yahaya Msigwa akiwa na wanajumuiya katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Kiislamu kilichopo Ilala manispaa ya Iringa. |
Viongozi wa Chama wilaya ya Mufindi wakiwa kijiji cha Sadani kwaajili ya mkutano wa Hadhara. |
Jamii mkoani Iringa imetakiwa kuunga mkono jitihada za serikali na wadau mbalimbali katika katika kwasaidia watu wa makundi maalumu hususani wezee na walemavu waliopo katika maeneo yao.
Imeelezwa kuwa kuwasaidia watu wa makundi hayo ni jukumu la kila mwanchi kutokana na hali zao na mahitaji waliyonayo ambapo itawasaidi kuwajengea matumaini mapya katika maisha yao kama wananvyo eleza Ashura Jongo kaimu mwenyekiti UWT mkoa wa Iringa na Cesilia Ismail katibu UWT wilaya ya Iringa walipotembelea kituo cha kulelea wazee cha MAKHAZINI kilichopo kitanzini Manispaa ya Iringa na kutoa msaada wa vyakula mbalimbali kituoni hapo.
Nao baadhi ya wanajumuiya hiyo ya wanawake wa CCM waliohudhulia katika ziara hiyo wamesema wataendelea kujitolea katika kuwasaidia wazee na wasiojiweza pamoja na kuendelea kwahamasisha wananchi kuunga mkono jitihada zinazofanywa na wanawake wa chama cha mapinduzi hasa katika kipindi hiki cha maadhimisho ya miaka 39 ya CCM.
Bi Hadija Tagalile ni mlezi wa wazee hao amesema wanawake waliopo kituoni hapo ni wale waliokosa msaada kutoka kwa ndugu zao japo katika kituo hicho wakiendelea kupata huduma huku baadhi ya wazee waliopokea msaada huo wakiendelea kuhamasisha jamii kuwatembelea katika kituo hicho.
Alhamisi, 21 Januari 2016
MBUNGE ROSE TWEVE:NITAPIGANIA MAENDELEO YA WANAIRINGA WOTE BILA KUJALI ITIKADI WALA DINI UONGOZI NI KWAAJILI YA WATU.
Zikiwa
zimebaki siku chache Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kuanza tayari
baadhi ya wabunge wameanza kuingia mkoani humo kwaajili ya maandalizi na
kukutana na wananchi wao na kupokea kero na mambo yanayotakiwa kupelekwa
Bungeni.
Wananchi wanayoshauku kubwa kutaka kuona mwenendo wa Bunge
hili la 11 chini ya usimamizi wa Spika wa Bunge Ndg.Job Ndugai na Naibu Wake Dr
Tulia Akson ambapo wanaamini litajaa hekima na Busara katika kujadili maswala
ya maendeleo ya wananchi bila kubagua aina ya mtu kutokana na aina ya kiongozi
wa nchi yaani Rais Magufuli kuonesha kuwa hana upendeleo na yupo kwaajili ya
kuwatumikia watanzania wote.
Hali hiyo inamfanya mbunge wa vitimaalumu mkoani Iringa
kuona umuhimu wa kuzungumzia suala la nini kitakachofanyika katika kipindi
chake cha miaka mitano ya awali ikiwa anatambua kuwa uongozi ni dhamana
aliyopewa kwaajili ya wengi,"ninaondoka Iringa kwenda dodoma nikiwa najua
changamoto na shida walizonazo wananchi wangu wa Iringa hususani wanawake
katika sekta mbalimbali Afya,Elimu,Maji,Miundombinu na huduma nyinginezo ambazo
kwahakika zinaumiza na kwa kutambua hilo nitafanya kazi kwaajili ya wananchi
jukumu langu kubwa nikuhakikisha nazifikisha changamoto zao mahali panapo
stahili na kuhakikisha zinatatuliwa"alisema rose
Aliiendelea kusema,"kwa muda mrefu sasa wananchi ambao
wametupa dhamana hii ya kuwaongoza wamekuwa wakiishi katika maisha duni ni kama
hawana viongozi inasikitisha pia kuona mkoa wa Iringa uliojaa raslimali nyingi
za misitu na mbuga za wanyama tukaendelea kuishi maisha yaleyele tuliyoishi
enzi hizo ni lazima tuhoji na wananchi wanufaike na mali zao haiwezekani mali
walizoshiriki kuzitafuta,kuzilinda mpaka zilipofikia halafu wakafaidi watu
wageni sasa ni mwenyeji kwanza mgeni baadae hilo ndilo jukumu langu kama
mbunge"alisema
Anasema kumekuwa na tatizo la wanawake wajawazito kukosa
huduma za kujifungua katika hospitali mbalimbali na vituo vya afya jambo ambalo
linatakiwa litafutiwe ufumbuzi huku akisema jukumu la wabunge ni kuihamnasisha
serikali kutenga bajeti itakayotatua baadhi ya kero hususani hiyo ya kuboresha
huduma za afya.
"pamoja na kutambua hali hiyo inayo wakabili wanawake
lipo pia tatizo la huduma hiyohiyo ya afya kwa wazee ambapo serikali ilitangaza
kuwa wezee watatibiwa bure lakini bado ipo changamoto kwa baadhi ya hospitali
na zahanati bado zinaendelea kuwatoza fedha wazee kazi yangu ni kwenda
kufuatilia sheria zinasemaje juu ya jambo hili" alisema rose
Endelea kufuatilia ujue mambo yatakayotekelezwa na Mh Rose
katika kipindi cha miaka mitano ya mwanzo...............asanteni.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)